MGAMBO wa
kituo cha polisi cha Nzera kilichopo Tarafa ya Bugando Wilayani Geita Mkoa wa
Geita wanatuhumiwa kuwaweka mfukoni polisi baada ya kumshambulia kwa kipigo
mwalimu msitaafu kisha kumvunja mbavu zake bila kukamatwa
mwalimu Samson akiwa amelazwa wodi namba 8 hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kujeruhiwa kwa kipigo.
Kufuatia hali hiyo wananchi wa Kijiji cha Nyamboge Katika kata ya Katoma
Wilayani Geita Mkoani hapa wamelituhumu Jeshi la polis Mkoani hapa kwa
kushindwa kumkamata mtuhumiwa aliyeusika kumpiga Samsoni Mzingwa(58) na
kumvunja mbavu zote na huku aliyefanya kitendo hicho hakiwa mitahani
hakitamba na kujigamba kuwa polis wemewekwa mfukoni mwake.
Tukio
hilo limetokea tarehe 14 mwaka huu
majira ya asubuhi wakati Mwalimu Samsoni
Mzingwa(58),akielekea shambani kwake.
Akizungumza
kwa shida Samsoni alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni yeye alikodiswa
shamba mwezi huu kwa ajili ya la kulima Maindi na Rukasi Bunzali pamoja
na Wiliamu Bunzali wote wakiwa ni wanafamilia moja kwa makubaliano ya kuwalipa
miliono moja na laki tanona kulipa pesa zote na kuanza kulima mala moja
kwa ajili ya kupanda mazao yakiwemo maindi na mahalage.
Lakini juzi wakati akienda shambani kwake alishutukia watu
wanne wakiwa na mgambo wawili wa kituo cha polis Nzera kilichopo katika wilaya
Geita wanamzingila na kuanza kushushia kipigo kikubwa hadi kumvuja mbavu huku
wakimtembeza uchi wa mnyama ali iliosababisha maumivu makali na kulazimika
kulazwa katika Hospitali ya wilaya ya Geita.
Alisema
kuwa pamoja na kuwatambua waliomfanyia kitendo hicho na kuwataja kwa majina
kuwa ni Masalu Mwnangwa na Kona Mwanangwa lakini wamewakamata mgambo na kona
wakati Masalu akizidi kutamba mitaani na huku polis wakiwa wanamuona lakini
awataki kumkamata uenda wanamuogopa kwa kuwa ana pesa alisema Samson.
Naye
Mtoto wa Mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Baraka Samsoni alisema kuwa
kuwa yeye alipata taalifa na kwenda kulipoti kwa OCS Nzera lakini akuna
kilichofanyika zaidi ya kuzunguswa na OCS huyo huku akiambiwa asiwafundishe
kazi asikali hao.
Mganga
mfawidhi wa Hoaptali ya Wilaya ya Geita Adam Sijaona amekili kumpokea mgonjwa
na kumalaza wodi No 8 na kusema baada ya kupiga Picha waliona wanasubili
majibu lakini vipimo vya awali vinaonyesha ameumia mbavu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni