Basi lenye namba T 846 la kampuni ya CITY BOY lililokuwa likitokea jijini Dar kwenda Kahama Mkoani Shinyanga likiteketea kwa moto eneo la Saranda Mkoani Singida jana(juzi).
Basi hilo liliokolewa na kondakta
ambaye baada ya kuona dereva wake amekimbia aliamua kuliondosha eneo
hilo huku likiendelea kuwaka moto na kwenda kulitumbukiza ndani ya bwawa
mita zaidi ya 300 kutoka eneo la tukio ambako kwa kushirikiana na
wananchi walifanikiwa kuzima moto huo kabla haujaleta madhara makubwa
kwa gari hilo(Picha zote na Victor Bariety aliyekuwa safarini akitokea
Dar kwenda Geita)



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni