SIKU chache baada ya
CCM kumpitisha Dk John Magufuli kuwa mgombea wake wa urais,baadhi ya wananchi wa wilaya ya Geita Mkoa wa Geita na
viongozi wa CHADEMA wamewataka watanzania kwa ujumla kutembea wakiimba
Ukawa kwanza Magufuli baadaye kwa kile
walichodai mgombea huyo wa urais kupitia
chama cha hicho anayetoka mkoani hapa hana jipya kwani hawezi kulketa mabadiriko yoyote.
Upendo Peneza akihutubia wakazi wa mji wa Geita katika viwanja vya stand ya zamani
Kutokana na hilo
wananchi hao wamewataka watanzania kuunga mkono vyama vinavyounda umoja wa
katiba ya wananchi(UKAWA),kwa kuchagua rais,mbunge na diwani anayetokana na
umoja huo kwani ndiyo tumaini ambalo litaleta mabadiriko ya kweli katika kuinua
uchumi na kuwafanya watanzania wafaidi raslimali zao ambazo kwa miaka mingi
zimekuwa zikiishia mifukoni mwa mafisadi wachache.
Wananchi hao walikuwa
wakitoa maoni yao baada ya kupewa fursa ya kuuliza maswali kwenye mkutano wa
hadhara ulioitishwa na mjumbe wa mkutano mkuu BAWACHA Taifa Upendo Peneza
ambaye pia ni mtia nia wa ubunge wa jimbo la Geita kupitia chama cha demokrasia
na maendeleo(CHADEMA)uliofanyika jana(juzi)uwanja wa stand ya zamani ya mjini Geita.
‘’Mimi sijasimama
hapa kuuliza swali,kwanza nikupongeze kwa hotuba yako nzuri ila mimi nilikuwa
nashauri watanzania wenzangu hususani wanaotoka katika mkoa wa Geita msije mkabweteka chama cha mapinduzi kuwateulia mgombea wa urais kutoka kwenu na
ninataka niwaeleze tu kwamba ndani ya chama cha mapinduzi(CCM), hata
akisimamishwa maraika tusitegemee mabadiriko yoyote’’
‘’Mnachotakiwa
kufanya kila mmoja wenu atembee akiimba
wimbo wa ukawa kwanza Magufuli baadaye na ndiyo njia pekee itakayopelekea
kuondokana na umaskini unaotukabili maana kama ameshatamka hadharani kwamba
hatawaangusha na atailinda ilani ya CCM,mnategemea nini hapo kwamba wezi
atawalinda maana ndiyo sera ya chama chao’’alisema Yukuri Yukuri huku
akishangiliwa.
Kwa upande wake
Peneza aliwataka wakazi wa jimbo la Geita kumuombea dua ili chama chake
kimteuwe kwenye kura za maoni na baadaye
kuwa mbunge wa jimbo hilo ili alete mabadiriko ambayo yamekosekana chini ya
wabunge wa chama cha mapinduzi(CCM).
‘’Iwapo nitachaguliwa
kwenye kinyang’anyiro hicho nitahakikisha uongozi wangu ni wa vitendo zaidi
siyo wa maneno maana kero zote zinazowakabili wanageita ni kutokana na makosa
ambayo mmekuwa mkiyafanya kila baada ya miaka mitano kwa kuchagua wabunge wa
CCM,huduma za afya mbovu,hakuna maji,wachimbaji hawana maeneo na wanapoibua
dhahabu wanafukuzwa,nitahakikisha hayo matatizo yanabaki historia ninaomba dua
zenu ili chama kiniteuwe na niwe mbunge wenu’’alisema Peneza huku
akishangiliwa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni