Na Victor Bariety,Geita
Wakati
Taasisi,mashirika,ya serikali na binafsi yakipiga vita ramli
chonganishi zinazosababisha mauaji ya vikongwe na albino,Mganga wa
kienyeji ameamua kujisalimisha katika kanisa la TAG na vifaa vyake
kuteketezwa kwa moto na viongozi wa kanisa hilo.
Mganga
huyo,Luhanga Mkakazi(70)mkazi wa Mtaa wa Mwatulole mjini Geita
amejisalimisha jana(Jumamosi)katika kanisa la TAG lililopo jirani na
nyumbani kwake baada ya kukerwa na shughuli za uganga kuhusishwa na
mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi(Albino).
Uamuzi
wa mganga huyo umekuja siku moja tu baada ya walemavu wa ngozi
kuadhimisha siku ya Albino duniani ambapo hapa nchini shughuli hizo
zilifanyika jijini Arusha na mgeni rasmi alikuwa Rais Dk.Jakaya Kikwete.
Aidha
akizungumza katika Ibada Maalumu ya kanisa hilo,Mkakazi amesema,ameamua
kuachana na uganga na kumrudia mwenyezi Mungu huku akidai kukerwa na
shughuli hizo kuhusishwa na imani za kishirikina zinazosababisha mauaji
ya Albino na Vikongwe.
Amesema
alianza shughuli za Uganga akiwa na umri wa miaka 34 kwa kutibu
magonjwa mbalimbali pamoja na kupiga ramli ili kutambua matatizo ya
wateja wake ambao wengine walikuwa wakifika kwake kutafuta dawa za
biashara.
Mchungaji wa TAG Sanyajuu mjini Moshi Alfredy Mtinda ambaye
alikuwa akiongoza ibada ya kumuombea mganga huyo amesema vifaa
vilivyoteketezwa ni pamoja na ungo,shanga,vibuyu vya dawa na nguo za
sughuli za uganga,huku akiwaomba viongozi wengine wa dini kueneza injili
na kuwaelimisha watu kuachana na uganga wa kienyeji.
Mwinjilisti
wa kanisa hilo,Samweli Magazi amesema tukio linaifundisha jamii
kuachana na imani potofu za kutumia viungo vya albino na badala yake
kumwamini Mungu.
Katika mkoa wa Geita,takwimu zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2007 walemavu wa ngozi(Albino) sita wameuawa,watatu wakijeruhiwa huku vikongwe waliouawa katika kipindi cha Mwaka jana ni
Mwisho.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni