ALIYEZIKWA KIEBOLA AIBUA UGONJWA MPYA GEITA
Na Eliud DaleiMajibu ya ugonjwa wa Bertha Boniface(25) aliyehisiwa kufa kwa
Ugonjwa wa ebola katika Hospitali ya Wilaya ya Geita Mkoani humu
mwezi Augosti mwaka huu yameibua ugonjwa mpya wa ‘Chikungunya’ ambao
unafanana na ugonjwa wa homa ya Dengue.
Boniface ambae aliletwa hospitalini hapo akiwa anatokwa na damu sehemu
mbalimbali za mwili wake,na kuharisha na kutapika damu ulizua mjadala
huku wengi wakidai ni Ebola na madaktari wa hospitali hiyo
wakishindwa kuubaini ugonjwa huo na kuamua kutuma vipimo wizara ya
afya na Ustawi wa Jamii.
Akitoa majibu hayo leo mgamga mkuu wa Mkoa wa Geita Joseph Kisala
alisema majibu ya Marehemu aliyehisiwa kuwa na Ebola yamekuja lakini
yanaonyesha kuwa hana ebola bali anaugonjwa uitwao 'Arthropod Borne
Viral Arthritis' unaoenezwa na Kirusi kiitwacho ‘Chikukunya’ na
ugonjwa huo unapatikana nchi za Australia na haujawai kufika nchi za
Afrika.
“Ugonjwa huu ni mgeni kabisa hata mimi nimeshangaa kwani sijawahi
kuusikia ,na ni ugonjwa hatari kama ilivyo Dengue”alisema .
Alisema kuwa ugonjwa huo unafanana na ugonjwa wa Dengue na unaenezwa
na mbu aina ya’ Indexegypt’ ambao wanauma mchana wanamabaka maupe na
meusi.
Alitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni “homa za mara kwa mara,udhaifu
wa mwili,kutokwa na vipele vidovidogo mwili mzima ,kutokwa na damu
sehemu za wazi kama mdomoni,Puani,pamoja na masikioni na kwamba dalili
hizo ni kama za Dengue’alisema Kisala.
Aidha alisema ugonjwa huo ulibainika nchi za Australia na haujawahi
kufika nchi za Afrika ,hauna tiba maalumu,ambapo aliwataka wananchi
kuendelea kujikiga kwani huenda ugonjwa huo uko Tanzania katika
makazi na maji yaliyotuama.
Alisema ugonjwa huo mpaka sasa umeua mtu mmja ,na hajapatikana
mwingine ambae ameugua toka alipofariki mgonjwa awali ambae alizikwa
na Halmashauri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni