MKUU WA KITUO ANUSULIKA KIPIGO GEITA.
15,09,2014.
MKUU wa
kituo cha polisi cha Nyamboge kilichopo katika kata ya Katoma Wilayani Geita
Mkoani hapa amenusulika kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kukutwa akitaka kufanya mapenzi na
mwanafunzi katika nyumba anayoishi mwanafunzi huyo.
Tukio hilo
limetokea jana majira ya saa tatu usiku ambapo wananchi wa kijiji hicho wakiwa
na marungu na mikuki waliweka mtego wa kumnasa mkuu huyo aliyefahamika kwa jina Moja la Venance kuwa ana tabia za
kumrubuni mwanafunzi huyo kwa mda mrefu.
Aidha akizungumzia
tukio hilo binti huyo Rozimery Kahindi
(17) anayesoma kidato cha nne alisema kuwa siku ya jumapili mkuu huyo wa kituo
alituma maaskali wawili wiki jana wakaenda kumkamata huku akidai kuwa hajui
hata kosa lake lakini akalazimika kwenda na alipofika hapo alianza kulazimishwa
kuwa anatembea na mwalimu wake ndipo alipokataa alianza kupigwa na kulazimishwa
kuandika maelezo ambayo hata yeye hayakumbuki hadi sasa hivi.
Aliendelea
kusema kuwa baada ya kukataa kuandika maelezo alipelekwa rokapu na mda mfupi
alifuatwa na askari mmoja kati ya wale waliomfuata anapoishi alianza kuandika
maneno ya kutoa kichwani mwake na kulazimsha kusaini lakini aliendelea kugoma
na alipigwa sana na kuamua kusaini kutokana na kutishiwa kufungwa na mara baada
ya kusaini aliitwa na OCS huyo na kumwambia aende Nyumbani lakini arudi jioni
ana shida naye ya muhimu sana lakini hakurudi kutokana na kuchoka na kipigo
alichokipata kituoni hapo.
Kutokana na
mkuu huyo wa kituo kutuhumiwa na mwanafunzi kuwa anamtaka kimapenzi ilibidi
awaambie wanafunzi wenzake na wananchi na baada ya hapo wakatengeneza mtego ili
wamnase.
Siku ya
jumapili jana mkuu huyo wa kituo alikwenda Nyumbani kwa mwanafunzi huyo na
kuomba wafanye mapenzi kwa kuwa wenzake anaoishi nao hawakuwepo lakini aligoma
kufanya hiyo mda mfupi wananchi waliokuwa wamemuona anaenda kwa binti
huyo walifika hapo na kufunga mlango kwa nje na kuanza kupiga mwano ambapo OCS
huyo alivunja malango na kutoKa nje lakini wanchi walifanikiwa kumkamta na
kuanza kumpiga ambapo aliokolewa na askali na kufikishwa katika kituo kikuu cha polisi cha Wilaya ya
Geita.
Badhi ya
wanakijiji waliokuwepo kwenye tukio hilo
walisema kuwa OCS huyo amekuwa na tabia mbaya sana kwa wanafunzi wanaosoma
katika shule hiyo kwa kuwatongoza na wakikataa anawasingizia kesi au ndugu zao
hivyo kuomba serikali kumchukuria hatua kali OCS huyo kwa kitendo hicho kiovu.
Diwani wa
kata hiyo Josephat Komanya alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kulaani vikali
kitendo hicho na kuwaomba wanafunzi wa kata hiyo kuendelea kuwataja viongozi
ambao wanawataka kimapenzi kwa nguvu.
Kamanda wa
jeshi la polisi Mkoni hapa Joseph Konyo alipopigiwa sm yake ya mkononi kuzungumzia
juu ya tukio hilo alikata na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno zaidi ya mara mbili
hakujibu .
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni