Ijumaa, 24 Oktoba 2014

AKATWA SIKIO NA MKWEWE WAKIGOMBEA FILIGISI

Na Victor Bariety,Sengerema 09/09/2014

Katika hali ya kushangaza,mkazi mmoja wa kijiji cha lushamba katika kisiwa cha yozu kata ya bulyaheke wilayani sengerema mkoa mwanza amejikuta akikatwa sikio  la kushoto na baba mkwe wake walipokuwa wakigombea filigisi  wakati wa chakula cha mchana .  

Mwenyekiti wa wa kitongoji cha yozu,Samwel Osango amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo lililotokea septemba 7 mwaka huu,majira ya mchana  na kumtaja aliyekubwa  na kisanga hicho kuwa  ni Amos  Machela[30] mkazi wa kitongoji hicho cha yozu.

Amesema kuwa siku ya tukio kijana huyo alitembelewa na baba mkwe wake Michael  Charles  kwa lengo la kuwasalimia kama ilivyo mira na desturi za kitanzania.

Amefafanua kuwa,baada ya kufika kwake  alimkalibisha mgeni  nyumbani kwake ndipo kijana huyo alimwamulu mke wake kuandaa kitoweo kwa ajili ya mgeni huyo(mkwewe).

''Wakiwa wanasubili chakula waliondoka na kuelekea baa kwa lengo la kubadilishana mawazo  kwani ni muda mrefu walikuwa bado hawaja onana''.

''Baada ya kutoka baa walirudi nyumbani ili wapate chakula ambapo walikuta chakula kiko tayari''

''Baadaye kijana huyo alitoka kidogo na kumwambia mzee akute anaendelea kupata na baada ya kijana huyo kurudi alikuta filigisi haimo kwenye bakuri na ndipo alipotaka kujua aliyekula filigisi ile na mzee huyo(mkwewe)alimjibu kuwa  ni yeye na ugomvi ulianzia pale''alisema Osango.

Amesema kutokana na majibu yale kijana huyo alichukia na kutamka hadharani kuwa mzee huyo alikuwa amemkosea.

''mila za kabira la wakulya filigisi huliwa na baba mwenye mji  wewe utakulaje''alisema Osango huku akinukuu maneno ya kijana yule.Kutokana na hali hiyo tafrani ilinza  huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa hana adabu ambapo kwenye ugomvi huo kijana huyo kukatwa sikio lake la kushoto.

Aidha kwa mjibu wa mwenyekiti huyo.baada ya kukatwa sikio alipiga makelele ambapo wananchi walifika kisha kuwaamua huku mke wa kijana huyo ambaye ni mtoto wa mzee huyo akikimbilia kusikojulikana ili kuficha aibu hiyo kabla ya wawili hao kusameheana na kuendelea na maisha yao kama kawaida.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni