NA ELIUD DALEI,GEITA 16/02/2015
WATU wasiojulikana wamemnyakua mikononi mwa mama yake Mtoto mchanga(albino),Yohana Bahati umri wa mwaka mmoja na miezi sita,mkazi wa kitongoji cha Ilyamchele,kijiji cha Ilelema wilayani Chato mkoani Geita,na kuondoka naye kusikojilikana huku wakimjeruhi kwa mapanga mama wa mtoto huyo.
Tukio hilo linalohusishwa na imani za kishirikina hata katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa udiwani,ubunge na Urais limetokea feb 15 saa 2 usiku wa kuamkia leo.
Kwa mjibu wa polisi mkoani hapa,Watu wanaodaiwa kufanya unyama huo walikuwa wawili ambao walivamia nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye kusikojulikana baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.
Kwa mujibu kamanda wa polisi mkoani Geita,Joseph Konyo,alisema tukio hilo limetokea saa 2 usiku wakati mama wa mtoto huyo,Ester Jonasi(30)wakati akiwa katika harakati za kuandaa chakula cha usiku.
Alisema watu hao wakiwa na mapanga baada ya kufika katika familia hiyo,wamteka mama yake na katika kunyang'anyana walilazimika kutumia mapanga kwa kumjeruhi mama wa mtoto huo.
Familia hiyo inawatoto watatu wote Albino ambapo wakati mtoto mwingine anatekwa kaka yake alikuwa kwa jirani anacheza na aliporejea nyumbani alikuta tukio limetokea.
"Katika purukushani za hizo waharifu hao walimjeruhi mama wa mtoto huyo..sehemu za Mikono,kichwani na begani.na amelazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Geita kwa matibabu"
"Kilichotokea ni kwamba watu familia ya mtoto huyo..inaishi porini ambako ni eneo la hifadhi ambako hapatakiwi kuishi watu..kutokana na mazingira hayo ilikuwa si rahisi sana kuwamakata hao watu"
Jonyo alisema pamoja na juhudi za wananchi na polisi kufika eneo la tukio hazikuzaa matunda kuwakamata watu hao na kwamba juhudi za kuwatafuta watuhumiwa hao zinaendelea na hivyo kutoa wito kwa wananchi kushirikiana kuwasaka watu hao.
"Tukio ambalo ni la kwanza katika mkoa wetu wa Geita..limetuweka katika mazingira magumu sana.lakini tumejipanga timu ya makachero inaendelea kuchunguza na kwamba tutahakikisha huyu huyo mtoto anarudi"
Aidha alisema baba wa mtoto huyo,Bahati Msalaba anashikiliwa na kwa uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo kwani wakati linatokea alikuwa nje anaota moto(Kikome).
"Tunamshikilia baba wa mtoto kwa sababu ya uchunguzi kwani wakati tukio linatokea baba wa mtoto alikuwa nje kwa hiyo kwa uchungzi wa awali tunamshikilia..Pia mtoto yule mwingine(Hakumtaja jina)amechukuliwa na wilaya kwa uangalizi kwani eneo hilo linamazingira magumu"alisema Konyo. Tukio ni la pili kutokea kwa kipindi kisichozidi siku 50 katika mikoa
Hili ni tukio la pili kutokea
katika kipindi kisichozidi miezi miwili ambapo Disemba 27,mwaka jana mtoto Pendo Emanule(4)wa Ndami Misungwi alitekwa na watu wasiojulika na hadi sasa bado hajapatikana wala watekaji wa mtoto huyo hawajakamatwa.
Mwisho.
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni