Jumatano, 18 Februari 2015

KIGOGO WA SERIKALI WILAYA YA GEITA AMTWANGA MTENDAJI WA KATA

 NA ELIUD DALEI,GEITA 10/02/2015

WAKATI watanzania wakianza kusahau tukio la aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Bukoba Albert Mnali la kuwacharaza viboko walimu wa shule za msingi,tukio jingine kama hilo limetokea tena Wilayani Geita Mkoani Geita baada ya mratibu wa Tasaf wa Wilaya hiyo kumjeruhi kwa kipigo mtendaji wa Kata na kusababisha alazwe akitibu majeraha.





 Mtendaji aliyejeruhiwa kwa kipigo ni wa kata ya Kamhanga Wilayani Geita,Mkoani Geita Sabin Bunzari Ndaki(45)ambaye kwa sasa yuko hoi katika hospitali ya Wilaya ya Geita baada ya kujeruhiwa kwa kipigo na Mratibu wa Tasaf Wilayani hapa Damian Aloyce kwa kilichodaiwa kugoma kutoa rushwa ya Tshs 500,000.

 Kutokana na kipigo hicho,kwa sasa Mtendaji huyo amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Geita wodi namba 5(Grade)akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa mkono wake wa kulia na kusababishiwa maumivu makali sehemu ya kifua na mbavu.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Deus Seif amethibitisha mtendaji wake kujeruhiwa na kulazwa na kuongeza kuwa,mbali na mtendaji huyo kudai alipigwa na mratibu huyo wa Tasaf anaziachia mamlaka husika za uchunguzi na ndizo zitakazobainisha ukweli.

 Akizungumza na Gazeti hili wodini hapo Mtendaji Ndaki alidai kuwa siku ya tukio Feb 09 saa 9 alasiri alifika ofisini kwa mratibu huyo ambaye ndiye mlezi wa kata yake kuomba apitishiwe Muhtasari wa kikao cha maendeleo ya kata yake(WODC)ili akachukuwe vifaa vya ujenzi wa maabara unaoendelea katani kwake. Alisema badala ya kupitishiwa Muhtasari huo,Aloyce ambaye ni mlezi wa kata hiyo,alimuomba rushwa y ash.500,000 ili kupitisha Muhtasari huo,ndipo alikataa na kumtaka amrudishie Muhtasari wake aurudishe kwenye kamati ya kata.

 “Nilipokuwa nachukua MuhtasarMezani kwake..alinisukuma nikaanguka chini na kuanza kumshambulia kwa kiti..alilenga kunpiga kichwani..katka kujihami nikaweka mikono kujikinga kichwa..ndpo nikapata jeraha kwenye mkono wangu wa Kulia”alisema. Alisema imekuwa kawaida kwa Mlezi huyo kuomba fedha wakati wa utekelezaji wa maukumu yake,ili kupitisha jembo Fulani kwa manufaa yake binafsi.

 “Sio mara yake ya kwanza kuomba fedha hata kipindi cha nyuma kwenye miradi ya TASAF alikuwa na tabia ya kuomba fedha..ili akupitishie” Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Geita,Dk.Adam Sijaona alithibitisha kumpokea mtendaji huyo akiwa kwenye hali mbaya lakini alipatiwa huduma ikiwa ni pamoja na kushonwa sehemu ya jeraha.

 “Tulimpokea saa moja hivi za jioni,alikuwa na jeraha mkononi ambalo linaonekana kuna kitu kimejeruhi..sijui kama alipigwa..au la.Mambo mengine tuwaachia polisi wachunguze zaidi nini kilitokea”alisema Dk.Sijaona. Diwani wa kata ya Kamhanga,Dionizi Bugali alisema Mtendaji alipewa Muhtasari huo kwenda kupishiwa na Aloyce kwa lengo la kwenda kununua vifaa vya ujenzi wa Maabara,lakini cha kushangaza jioni alipata taarifa za mtendaji huyo kupigwa.

 Alisema kitendo kilichofanywa na Mlezi huyo kinakatisha tamaa”Tumechangisha michango kwa wananchi kwa ajili ya Maabara.Lakini kama hali hii inkatisha tamaa kabisa,na sisi tunamba vyombo vya dola vimchukulie hatua kali” Diwani huyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Maendeleo ya kata(WODC),alisema tabia ya mlezi huyo haifai na kwamba aliomba mkurugenzi amhamishe asiendelee kuwa mlezi katika kata hiyo,ili asikwamishe zoez la ujenzi wa Maabara.

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita,Des Seif alithibitisha mtendaji huyo kujeuhiwa na kwamba kilichotokea ni kwamba mlezi alipopewa Muhtasari ili kuupitisha aliutilia Mashaka na kumuomba atarudi baadaye ili kumpitishia ndipo ulitkea ugomvi.

 Alisema mtendai hakutaka Kuuacha Muhtsari huo kwenye ofisi ya Aloyce na ndipo walianza kuvutana na mtendaji akwa amechanwa na msumari kwenye mkono wake. “Mimi niliwaita wote wawili baada ya kupata taarifa zao,mtendaji anasema alipigwa na kiti lakini Mtuhumiwa(Aloyce),amesema kwamba muhtasari ule ulikuwa na makosa akamuomba auache wa kuwa likuwa na wageni..ataurudia baadaye..sasa hakukubali mtendaji wakaanza kuvutana akawa amechanwa na msumari..ndiyo Maelezo yao”alisema Seif.

 Aidha alisema sio uaratibu kwa mtumishi kuomba rushwa katka kutoa huduma,na ni kinyume cha sheria za utumishi wa umma na kuwaonya watumishi wengine katika Halmshauri hiyo kuacha tabia hiyo mara moja na kusisitiza uzingaia maadili.

Kwa upande wake mratibu huyo,Aloyce alipotakiwa kujibu tuhuma zinazomkabiri alimtaka mwandishi wa habari hizi kuonana na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kile alichodai yeye si msemaji wa sakata hilo. Mwisho.

MWISHO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni