SHUGHULI za uzalishaji mali mjini Geita juzi zilisimama kwa muda wakati mwanasheria wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA),Tundu Lissu alipowasili mjini hapa na pia wakati wa kumaliza mkutano wake wa hadhara.
Lissu,ambaye aliongozana na viongozi mbalimbali wa chama hicho Mkoa,Jimbo na Wilaya,aliwasili mapema juzi akitokea Biharamlo na kupokewa na maelfu ya wafuasi wa chama hicho pamoja na viongozi.
Maelfu ya wananchi walijitokeza kumpokea njia panda ya Kakola Geita iliyopo mtaa wa nyankumbu kata ya Nyankumbu nje kidogo ya mji wa Geita ambapo waliongoza msafara huo hadi ofisi za chama hicho jimbo la Geita zilizopo mtaa wa misheni mjini hapa.
Katika njia zote walizopita iliwalazimu wananchi kusimamisha shughuli na kuingia na kuingia barabarani ili kupata fursa ya kumuona Lissu.
Mbali na kusimamisha shughuli,barabara zililazimika kufungwa kwa muda kutokana na wananchi kutembea kwa miguu ,wakisindikiza msafara huo hadi hadi zilizo ofisi za chadema huku wakiimba dawa ya Pombe imewasili Geita,hatutaki Pombe tunataka UKAWAA.
Baada ya kuwasili ofisini hapo aliweka kumbukumbu kwenye kitabu cha wageni kisha kuelekea ukumbi wa kanisa katholic la mjini Geita alikowapa semina wanachama na viongozi wa chama hicho na baadaye maandamano hayo yalielekea uwanja wa mpira wa Nyankumbu nje kidogo ya mji wa Geita kisha kuwahutubia wananchi.
Akihutubia maelfu ya wananchi wa Geita,Mwanasheria huyo mkuu wa Chadema,Tundu Lissu,alitoboa siri ya Ukawa Kuchelewa kumtangaza mgombea wa Urais.
Alisema Ukawa umechelewa kumtangaza mgombea wa Ukawa kutokana na kwamba bado mgombea mwenza kutoka Zanzibar hajapatikana.
Lissu akiwahutubiwa wananchi wa mji wa Geita Juzi alisema kwamba mgombea wa ukawa anafahamika ndani na nje ya nchi na kinachosubiliwa ni kutangaza jina lake,baada ya taratibu zinazosubiliwa na umoja huo kukamilika na kwamba chama hicho kimesema hakitashindwa kwa goli la mkono.
Kauli ya Lissu ambaye ni Mbunge wa Singinda Mashariki aliitoa alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi wa Mji wa Geita juzi waliokuwa wamefurika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Nyankumbu na kuufunika mkutano wa mgombea urais wa CCM ambaye pia anatokea Mkoani hapa John Pombe Magufuri.
Alisema Ukawa umechelewa kumtangaza mgombea Urais kutokana na kwamba mgombea mweza kutoka Zanzibar bado hajapatikana.
“Ndugu wananchi Mgombea wa Ukawa nimtaje..nisimtaje,aliwauliza wananchi waliofurika kwenye mkutano huo,Nao wakaitia mtaje’’Tumeshampata mgombea urais wa Ukawa..na mnampenda sana…na mnamjua sana…ni mtu anayefahamika nchi nzima na duniani kote”alisema Lissu huku akishangiliwa na wananchi.
Bila kumtaja jina lake,alisema Ukawa umeshindwa kumtaja jina kwa sababu bado mgombea mwenza hajapatikana na kwamba taratibu za kumpata ziko mbioni kukamilika.
Huku wananchi wakiwa na Shauku ya kutaka kujua jina lake(Mgombea wa Ukawa),Lissu alisema baada ya taratibu za kumpata mgombea Mwenza kutoka Zanzibar zitakapokamilika atatangazwa.
“Siku tunamtangaza Mtajua tu,Tukimpata Mgombea Mwenza
kutoka Zanzibar,Tutaita vyomvo vyote vya habari,Televisheni zote ili kumtangaza kwa hiyo mtamjua”alisema Lissu.
Hata hivyo Umati wa wananchi uliokuwa umefurika uwanjani hapo ulizizima kwa Kushangilia baada ya Mwanasheria huyo wa Chadema alipojikuta akimtaja Dk.Willbroad Slaa wakati akitoa ufafanuzi wa sababu zilizochelewesha kumpata mgombea wa Umoja huo.
“Kuna mambo yametuchelewesha kumtangaza Dk.Slaa’’na Wananchi walizizima kwa kushangilia na kukatisha hotuba yake baada ya mwanasheria huyo kujikuta akimtaja mgombea wao bila kutarajia,na mkutano ulipotulia aliendelea”Samahani Ulimi hauna Mfupa samahani sana naomba mniwie radhi jamani”alisema Lissu na kuibua vicheko kutoka kwa wananchi hao
Alisema Umoja huo hauwezi kufa mbali na baadhi ya Viongozi wa serikali na vyama vya Siasa ikiwemo CCM ambao wana uombea Ukawa Uparanganyike.
“Wapo wanaotuombea mabaya Ukawa na wengine wanapewa fedha ili kuhakikisha Ukawa unavunjika,Kamwe Ukawa hautavunjika…nawahakikishia wananchi kwamba Ukawa uko Imara na hautavunjika hata wakituombea mabaya”alisema Lissu na kuongeza.
“Akipatikana mgombea Mwenza wa Ukawa Kutoka Zanzibar,tutawazungusha nchi nzima kwa ndege kuwatambulisha..na mwaka huu hakuna jimbo likalopita bila kupigwa CCM tunao mguu kwa mguu,Mkoa wa Geita waliojitokeza kugombea Ubunge wako 31 na kwa nchi nzima wako 900”
Kuhusu Dk.Magufuli
Lissu alisema Ukawa hautishiki na Mgombea urais wa CCM,Dk.John Magufuli kwa sababu hajawahi kuzungumzia kero zinazowakabiliwa wananchi yakiwemo mateso yaliyowapata wafugaji baada ya ng’ombe zao kuuawa na wengine kuteswa wakati wa Oporesheni tokomeza.
Alisema tangu kuibuka kwa tuhuma mbalimbali dhidi ya serikali iliyopo madarakani likiwemo sakata la Richmond na Tegeta Escrow Dk.Magufuli hajawahi kusimama na Kuutangazia umma wakiwemo wananchi wa Geita nini msimamo wake kuhusiana na kashifa hizo.
“Dk.Magufuli anamsimamo gani kuhusu Tegeta Escrow,Richmond,oporesheni tokomeza ilikuja badala ya Kushughulikia majangili wakashughulikiwa wafugaji,na Magufuli hajawahi kujitokeza kusema lolote kuhusu ng,ombe zilizouawa huku Biharamulo”
Alisema dalili za Chama cha CCM kushindwa mwaka huu zinatokana na mchakato wa kumpata mgombea Urais wake kutawaliwa na Mizengwe ambapo kamati ya Maadili isiyokuwa na maadili ilisababisha kupigwa mabomu ya machozi wafuasi wa CCM huko Dodoma mabomu yaliyokuwa yamezoeleka kwenye Mikutano ya Chadema.
“Serikali ya CCM imeshindwa hata kutupatia Katiba,Wabunge wa CCM wamepitisha Mswada wa Sheria ya Mafuta na Gesi yenye lengo la kuwaumiza wananchi”
‘’Sasa hivi wamewaletea Pombe kuwahadaa watu wa kanda ya ziwa kwamba wameleta mtu wa kabila yao,nataka niwaambie kuwa Pombe si msubi,Musukuma wala mzinza kama mnavyoaminishwa watu wa kanda ya ziwa ambao mmeasi na kuikataa CCM’’
‘’Kabila ya Pombe ni CCM,akikutana na watu wa kabila yake kina Kikwete,Mangula,Mkapa wanaongea kabila moja,na ndiyo maana pamoja na wagombea wenzake kina Pinda wakati wakisaka wadhamini walidai watapambana na rushwa lakini Magufuri hata siku moja hakuwahi kukemea rushwa wala kujinadi kwamba atapambana na rushwa kwa sababu kabila yake imeapa akuilinda na kuitetea’’alisema huku akishangiliwa.
Awali Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita,Alphonce Mawazo alisema Dk.Magufuli ha na jipya kwa Watanzania wala Chadema hakiwezi kuteteleka kutokana na kwamba ndani ya CCM hakuna msafi anayeweza kumaliza matatizo ya wananchi.
Alisema wachimbaji wadogo wa Geita kila kukicha wanahangaika kutafuta maeneo ya kuchimba bila mafanikio huku maeneo mengi yakiwa yamehodhiwa na wachimbaji wakubwa hali inayowafanya wachimbaji hao kuishi kwa kutanga tanga.
MWISHO.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni