Jeshi la
polisi Mkoani Geita limemkamata mstaaf wa jeshi la wananchi Tanzania
kikosi cha Komando sajent Mathias Christopher Etta(55)kwa tuhuma za
mauaji ya mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu.
Etta pia ni msimamizi msaidizi wa kampuni ya ulinzi ya (Nguvu
moja security service) inayofanya shughuli zake za ulinzi kwenye mgodi wa
madini wa Bacreef uliopo maeneo ya Lwamgasa mkoani hapa.
Sajent Etta
alitiwa nguvuni jana majira ya saa 8 mchana kwenye kituo kidogo cha polisi cha
Bacreef baada ya mwili wa marehemu Yona Onesmo (35) ambae ni mkazi
wa kijiji cha Isingiro kata ya Lwamgasa na mchimbaji mdogo kukutwa umetupwa
pembezoni mwa barabara karibu na daraja la kijiji cha Mnekezi umbali wa
kilomita (2) kutoka Lwamgasa na kilomita
takribani (15)kutoka Hospitali ya Katoro alikokua amepelekwa
kupatiwa matibabu.
Imeelezwa na mashuhuda wa tukio hilo kuwa,baada
ya kupigwa usiku wa kuamkia julai 30 mwaka huu na walinzi wa kampuni
ya( Nguvu moja) kwa kosa la kukutwa wanachimba kwenye eneo lililozuiliwa la
mgodi wa Bacreef alikimbizwa hospitalini kabla ya mwili wake kukutwa pembezoni mwa Barabara itokayo Katoro
kwenda Lwamgasa majira ya saa nne asubuhi baada ya wakazi wa kijiji cha
Mnekezi kupewa taarifa na wapita njia ukiwa bado una (Kanyura) za
Hospitali zinazotumika kutundikia drip za maji.
“Kiukweli Katoro kwenda kutibiwa”alisema afande
Samweli Yusuph wa kituo hicho aliyeutambua mwili huo baada ya kufika eneo
la tukio.nashangaa amefikafikaje hapa kwani jana mimi nimewapeleka Hospitali ya
Mganga mkuu wa Hospitali ya Katoro Dk Daniel Izengo
alionyesha kushangazwa na taarifa hiyo kwani alikua bado hajapokea
taarifa yakupotea kwa mgonjwa hospitalini hapo,licha ya ( postmotam)yaani kikao
cha wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwa tayari kilikuwa kimeshafanyika.
Hali hiyo
ilimlazimu Dk,Izengo kumtafuta mhudumu aliyekuwa zamu Dk,David Mgalula ili
kuzungumzia kizungumkuti hicho,akitolea ufafanuzi mhudumu huyo alikili
kuwapokea wagonjwa hao wawili Bwana (Onesmo na Ndagicheye) nakusema kuwa hali
ya Bw,Onesmo haikuwa nzuri kwani Marehemu alidai kuwa anajisikia maumivu makali
tumboni.
“Nikweli niliwafanyia uchunguzi wa awali (Physcal
chekup)nikabaini walikua na michubuko mikononi,usoni pia
walikua wamevimba joint ila marehemu alidai kuwa tumbo linamuuma
nilimwandikia sindano za masaa 6 aina ya(X-pen) Sindano za Tetenasi na dawa
zakumeza aina ya (Dicrofenaki)kila baada ya masaa 8 pamoja na drip,mwenzake
aliruhusiwa kwani alikua anajisikia vizuri,sasa nashangaa kwanini marehem aliamua
kutoroka,labda alihofia kushitakiwa na Mgodi wa Bacreef”alisema Dk huyo.
Kwa upande wa Sajent Hamis Kabonga ambaye ni msimamizi mkuu wa
kampuni ya ulinzi ya (Nguvu moja security service ) alikiri kushikiliwa
kwa msaidizi wake nakuongeza kuwa kukamatwa kwake kunatoka na utata wa kifo cha
Yona onesmo ambae alikua nimiongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa julai 30 saa 11
kwa ajili ya kufikishwa mahakamani mara baada yakutibiwa.
Hata hivyo
hakuwa tayari kuzungumzia uwepo wa migogoro ya mara
kwa mara kati ya kampuni hiyo ya uchimbaji ya Bacreef na wananchi wanaozunguka
mgodi huo kwa madai kuwa msemaji wa kampuni hiyo yuko safarini hadi pale
atakaporejea.
Aidha uchunguzii wa gazeti hili umebaini kuwa,licha ya kamati ya
ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita kukutana na pande hizo mbili mwanzoni mwa
mwaka huu kati ya April na Mei mwaka huu ili kutatua migogoro hiyo,bado matukio
yenye utata yanaendelea kujitokeza mgodini hapo.
Kwa upande
wake kaimu kamanda wa polisi Mkoani Geita,Peter Kakamba amethibitisha
kushikiliwa kwa mstaaf huyo wa jeshi la wananchi Tanzania kwa
mahojiano zaidi.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni