Jumanne, 11 Agosti 2015

WAGOMBEA SABA CCM GEITA KUMFUATA LOWASSA?



NA VICTOR BARIETY,GEITA

Wagombea saba wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi wamepinga matokeo ya uchaguzi kwa madai kwamba yamegubikwa rafu na karatasi za kupigia kura kutokuwa na picha za wagombea huku wakitishia kufanya maamuzi magumu iwapo malalamiko yao yatapuuzwa.


Pia wamedai kwamba jina la mgombea mmoja la Juma Malunga ambaye alijitoa katika kinyang’anyiro jina lake likikuwepo katika karatasi za kupigia kura na kupata kura 184 ambaye hata hakupiga kampeni.

Wagombea walijitokeza kupinga matokeo hayo na kura zao katika mabano ni Paschali Malugu(2,253)ambaye amekuwa wa pili mbele ya Contantine Kanyasu aliyetangazwa mshindi kwa kura 2,553.

Wengine ni Jacob Mtalitinya(1,249),Evarist Nyororo(1,187),Dk.Lonard Mugema(410),Dk.Daffa Mohamed(213) ,Juma Malunga(184),Seif Kulunge(158),Regina Mikenzi(251),na Dk Samweli Opurukwa(218).

Aidha wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,Mkurugenzi wa Uchaguzi CCM wilaya ya Geita,Kilian Balindo katia ya watia nia 10 waliojitokeza kwenye mkutano wa kutangaza matokeo hayo walikuwa watatu tu,Mikenzi na Merikiory pamoja na Kanyasu,huku idadi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kusikiliza wakiwa wachache sana.

Akizungumza kwa niaba ya watia nia wenzake,Dk.Opurukwa alisema wanapinga matokeo hayo kwa kutokana na Zoezi zima la upigaji wa kura za maoni Agosti Mosi kukubigwa na rafua za rushwa na baadhi ya viongozi kuwapigia debe baadhi ya wagombea.

“ kwanza karatasi hazikuwa na ubora,tulitarajia kuwa na picha za wagombea,karatasi zilikuwa hazina picha,wagombea tuliokuwa tunafahamika tulikuwa kumi,lakini wagombea waliojitokea 11,wagombea wawili majina yao yanafafana kwa karibu sana ambapo kufanana kwa majina hayo yanawezea kuwachanganyanya wapiga kura”alisema Dk.Opurukwa.

Alisema dosari zingine zilijitokeza katika Kata ya Mugusu ambako kulitakiwa kuwa na wapiga kura 300 lakini walkiojitokeza  kupiga kura walikuwa  747 na Tawi la Machinjio wapiga kura walikuwa 300 waliopiga kura 350.

“Dosari zingine ni kadi za  wana ccm zilizokuwa zinatakiwa kupigiwa kura hazikuwa na picha na zingine zilikuwa hazijalipiwa ada”alisema msemaji wa watia nia hao.

“Kata ya Bung,wangoko,Bulela mambo hayo yalijitokeza sana,Dosari ya tano katika kufanya majumuisho kutoka kwenye vituo,hakukuwa na wawakilishi wa wagombea,dosari nyingine mmoja wa wagombea aliweza kuweka bango lenye picha yake na picha ya mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais”alisema Dk.Mugema

“Kwa maana ya kwamba mgombea huyo alikuwa ametumwa na mgombea urais,ambapo aliweka mabango sehemu mbalimbali akiwaaminisha kwamba yeye ndiyo mgombea pekee na anayefaa.
Alisema kwa ushahidi walioupata  baadhi ya viongozi wa chama walikuwa wakimpigia debe mgombea mmoja,Tumeandika barua yetu tunasubiri”.

Wagombea hao wameandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa Uchaguzi na nakala kwa ofisi ya mkoa na makao makuu ya CCM Taifa.

Akizungumzia malalamiko ya wagombea hayo Mkurugenzi wa Uchaguzi alisema katika zoezi la uchaguzi hakuna dosari iliyojitokeza.

Alisema malalamiko yao hayana ukweli wowote na kwamba hakuna barua walioyoipokea kutoka wa wagombea hao.

“Mimi sijapata malalamiko,hadi natangaza matokeo muda huu hakuna barua iliyotumwa ya kulalamika”alisema Balongo.

Matokeo katika jimbo la Geita Vijijni,aliyeshindwa Joseph Msukuma 9,699,Ernest Mabina(1,501),Thomas Ntogwakulya 811,Pima Marko 461 ,Luponya Sherembi 408,na Sabato Vitusi(107).

Busanda aliyeshinda Lolesia Bukwimba kwa kura 13817,Tumaini Magesa kura 6363,Sostenes Kulwa 1858,Fransic Kiganga 1150,Luchenhe Mbatilo 134,na Mhonzu John 117,na Malembeka Mark 96.

Jimbo la Chato,aliyemridhi Dk.John Magufuli ni Dk.Merdadi Kalemani 12,892,Deusdedit Joseph 3,251,Simon Michael 2,150,Dk.Alphonce Chandika 1,244,Revocatus Alex 661,Luge Ismail 539,Aman Shaaban 538,Majura Kasika 369,Michael Jigabha 348,Mkinga Mkinga 321 na Yohana Nasorro 111.
Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni