NA ELIUD DALEI,GEITA 13/02/2015
Chama cha demokrasia na Maendeleo(Chadema),kimesema kikiingia madarakani kitaifuta katiba pendekezi ikipitishwa,na badala yake kitatumia katiba iliyokuwa imependekezwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba,Jaji Joseph Warioba.
Akiwahutubia wananchi wa Mji wa Geita,naibu katibu mkuu wa Chadema,upande wa Zanzibar,Salim Mwalimu alisema mkakati wa chama hicho ni kuingia Ikulu kwa kuwa kinaungwa mkono na wananchi wengi.
Mwalimu alisema Katiba ya warioba ilikuwa na lengo la kuleta mabadiliko ya uwajibikaji kwa viongozi wa umma,lakini kwa kutambua hivyo ccm waliona haifai na kuambua kuibadilisha.
Alisema chadema kitawahamasisha wananchi nchi nzima kwasihudhurie kwenye vituo vya kuipigia kura katiba pendekezi ili ipitishwe na CCM pekee yake kwa maslahi yao binafsi.
"Si mnaenda msikiti,na makanisani,kwani shekhe au mchungaji na padri wanawaununulia nguo ili kwenda kanisani au mskitini?..mnanunuliwa chakula ili kwenda kanisani na msikitini..kinachotakiewa sasa ni kuacha kwenda kupia kura"
Alisema Chadema kinazunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura na wala hakihamasishi wananchi kuipigia kura katiba.
"Janja yao tumeshaijua..kila kona tumewabana mbele,nyuma na katikati,hakuna pa kwenda..kwa hiyo ukifika muda wa kujiandikisha mkajiandikishe kwa wingi kwa ajili ya uchaguzi mkuu oktoba"alisema na kuongeza.
"Tume inataka kuleta jeuri ya CCM kwamba siku za kujiandikisha kila kanda ni siku saba tu..hata kama ni siku moja vyovyote itakavyokuwa nendeni tu mkajiandikishe kwa wingi hao hawana ujanja".
Katika mkutano huo aliwataka vijana wenye nia ya kugombea ubunge na udiwani kwenye maeneo yao kujitokeza kuomba nafasi hiyo,lengo likiwa ni kuhakikisha taifa linakombolewa.
Mwalimu Alisisitiza kwamba Chadema kipindi hiki hawatapokea makapi kutoka chama cha ccm,na badala yake kinatumia vijana wa Chadema wenye nia ya kweli kuwatumikia wananchi.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni