NA VICTOR BARIETY,GEITA 18/02/2015
Wananchi wa mji wa Geita jana(juzi),waliingiwa na Hofu kubwa,huku watu wanane wakazi wa Mtaa wa Katoma wakinusurika kufa kwa kupoteza fahamu baada ya kutokea Mlipuko Mwingine mkubwa ambao haujawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita GGM wakati wakilipua miamba ya dhahabu.
Tukio hilo limetokea majira ya saa tano asubuhi ambapo baada ya kutokea hali hiyo watu waliokuwa majumbani,maofisini walitoka nje kwa hofu na wengine wakikimbia huku na kule kuokoa maisha yao wakidhani ni magaidi yamevamia mji wa Geita.
Hali hiyo ilisababisha watu sita kuzumia huku wawili kati yao,ambao ni Rose Pastory(49),na Markiana Shamba(42) wakikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kuokoa maisha yao na baadaye kulazwa baada ya kuanguka na kupoteza fahamu muda mfupi baada ya kutokea kwa mlipuko huo.
‘’Nilikuwa nimekaa nikasikia mshindo mkubwa na dipo nikadondoka chini na kupoteza fahamu nimekuja kuzinduka nipo katika hospitali’’
''Kwa kweli wananchi wa katoma tumeshateseka sana kana kwamba hatuna viongozi wanaoweza kutusemea matatizo yetu,mimi hii ni mara ya pili napoteza fahamu na kulazwa hapa hospitali’’
‘’Kuna wakati nilizimia na kulazwa hapa,mkuu wa wilaya akija anatuhadaa kwamba hakuna madhara ambayo yanaweza kutupata akitoka wanalipua,namuomba Rais Kikwete kama kweli ni muumini mzuri wa dini ya kiislamu asikie kilio chetu au mpaka asikie katoma kumetokea maafa makubwa ndiyo wachukuwe hatua?’’alihoji,Markiana Shamba ambaye amelazwa wodi namba 8 grade
Kwa upande wake,Rose Pastori mwathirika wa milipuko hiyo ambaye pia amelazwa katika wodi hiyo alidai wakati mlipuko huo unatokea alikuwa dukani kwake akihudumia wateja na ndipo aliposhituka akidondoka chini na kupoteza fahamu ambapo alizinduka akiwa hospitalini hapo.
Aliitupia lawama Serikali ya Wilaya hiyo kupuuza malalamiko yao ya muda mrefu kutokana na milipuko hiyo jirani na makazi ya watu na kudai kuwa iwapo itaendelea kuwapuuza na kuligeuza suala la kisiasa kama inavyofanya hivi sasa ijiandae kwa maafa makubwa.
‘’Unajua huu mtaa wa katoma kwa miaka mingi imekuwa ngome ya CHADEMA na ndiyo maana hata tunapotoa kilio chetu hatusikilizwi na limegeuzwa suala la kisiasa na hata tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya ya Geita Manzie Mangochie kushughulikia malalamiko yetu ipo kiulaji zaidi na hakuna inachokifanya na sasa serikali inatuandalia kifo watu wa katoma’’alisema Bi,Pastori
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Geita Dk.Adamu Sijaona akathibitisha kuwapokea wahanga wa Tukio hilo ambao wakati wanafikishwa hospitali hapo walikuwa hawajitambui.
Ofisa Mahusaino wa Mgodi huo Josepha Mangilia hakutaka kuzungumza kitu chochote na badala yake kumtaka Mwandishi wa habari kwenda kumuona Mwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia kero za watu wa katoma.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo iliyoundwa na Mkuu wa wilaya ya Geita Manzie Mangochie kufuatilia migogoro ya watu wa katoma alisema anafuatilia suala hilo.
Kwa upende wake mwenyekiti wa Mtaa wa Katoma Patrick Faida amesema kamati iliyoundwa haiwanufaishi watu wa Katoka na badala yake imekuwa ya kisiasa na kwamba inatakiwa kuvunjwa hata kama ni kwa nguvu ya umma.
‘’Hii kamati ya mkuu wa wilaya imetengenezwa kwa ajili ya watu kujipatia ulaji,nimeshamfuata mkuu wa wilaya kumtaka ivunjwe na iundwe nyingine akanijibu sina mamlaka ya kumhoji na kwa sasa nimejipanga kuitisha mkutano wa hadhara na umma ndiyo utaamua cha kufanya juu ya kamati hiyo hata ikibidi umma kuivunja tutafanya hivyo ili kuokoa wananchi wetu’’alisema Faida.
Hata hivyo baadhi ya wanaharakati akiwemo Mussa Mabina ambaye ni mwenyekiti wa IRS asasi ya kiraia inayohusika na masuala ya vijana na watoto aliiomba Kampuni ya Geita GGM,Serikali na wananchi wa katoma ambao wamekuwa wakikumbwa mara kwa mara na matukio ya Vifo na kuzimia kutokana na kuwepo kwa mgodi huo kukaa meza kuondoka kero hizo.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni