Alhamisi, 11 Septemba 2014

majambazi yafanya kufuru

MAJAMBAZI YAFANYA KUFURU GEITA


Na Eliud Dalei,Geita 06/09/2014

SIKU chache baada ya mkuu wa mkoa wa Geita Magalula Said Magalula kutoa tambo akiwatahadharisha majambazi watakaoingia Geita kutotoka salama,hali imekuwa tofauti baada ya majambazi kuingia na kuvamia kituo cha polisi Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita na kuua Askari wawili na wengine wawili kujeruhiwa kisha kupola bunduki kumi risasi na mabomu ya mkono kisha kutokomea pasipo kukamatwa.

Magalula alitoa tambo hizo hivi karibuni muda mfupi baada ya majambazi wawili kumuuwa kwa kumpiga risasi wakala wa M-pesa wa mjini Geita Gosbert Walwa kisha kupora fedha kabla ya majambazi hao kuuawa na polisi kwa kushirikiana na wananchi wa Wilaya ya Nyang'hwale mkoani hapa tukio lililotokea majira ya jioni.

Katika tukio la leo(jana)septemba 9 mwaka huu,majambazi hao walivamia katika kituo kikuu cha polisi Wilaya ya Bukombe Mkoani hapa saa 9 alfajiri wakiwa na siraha za kivita na mabomu ya kurusha kwa mkono.

Imeelezwa kuwa baada ya kufika kituoni hapo,majambazi hao walizingira kituo hicho hadi eneo la mapokezi(CRO)na kuanza kuwamiminia risasi za moto askari waliokuwa zamu(ulinzi kituo).

Katika hatua za awali Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa 9.45 alfajiri katika kituo cha polisi wilaya bukombe ambapo majambazi wamevamia kituo wakiwa na siraha nzito huku wakitumia bomu kwa kupiga dirisha la CRO na kuingia na kuanza kuwamiminia Risasi Polisi Waliokuwa Zamu. .
Kufuatia hali hiyo askari wawili kati ya wanne waliokuwa kituoni hapo walipoteza maisha huku wengine walkijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao.

Mganga mkuu wa wilaya ya Bukombe Dr Honorata Rutatinisibwa amekiri kupokea miili ya askari wawili wa kike na kiume.

Amewataja majina yao kuwa ni pamoja na WP 7106 PC Uria Mwandiga na askari namba G.2615 Pc Dustani Kimati.
naye mganga mkuu wa wilaya ya Bukombe DR Honorata Rutatinisibwa amekiri kupokea marehemu wawili wakike mmoja na wakiume mmoja ambao majina yao kuwa ni WP 7106 Uria Mwandiga na askari namba G.2615 Pc Dustani Kimati.

Dr Honorata amewataja askari waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwenye namba E.5831 CPL David Ngupama Mwalugelwa aliyejeruhiwa kichwani na usoni na kwamba ameumizwa vibaya sehemu za midomo yake huku meno mawili yaking'oka.

Mwingine ni Mohamed hassani kilomo amabye amejeruhiwa kifuani na mguu wa kulia uliovunjika mfupa kwa kupigwa Risasi.

Kwa mjibu wa Dr  Honoratha kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya wamewapa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio na kuahidi kutoa taarifa zaidi mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Hili ni tukio la tatu kwa askari wa kituo hicho kuuawa na majambazi ambapo Juni 28,2009 kundi la majambazi saba wenye silaha za moto aina ya SMG, yaliteka magari manne ya mizigo katika pori linalounganisha maeneo ya Lunzewe, Matabi na Buselesele lililopo Wilaya ya Bukombe, mkoani Shinyanga na kumuua kwa kummiminia risasi nne kifuani, askari polisi aliyejulikana kwa jina moja la Pascal wa Kituo hicho cha Polisi Bukombe.

Tukio hilo la kinyama lilitokea majira ya saa 1:15 asubuhi, ambapo huku yakitumia lori lililokuwa limebeba mkaa, yaliziba barabara inayokatiza katika pori hilo wakati Pascal na mwenzake wakisindikiza magari hayo ya mizigo kupita katika pori hilo.

Aidha hivi karibuni Bunduki ya kivita aina ya SMG Yenye namba BF 6697 na risasi 11 ilikutwa imetelekezwa nyuma ya nyumba karibu na bafu la kuogea kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Imalabupina kijiji Namalandula Wilayani Bukombe Mkoa Geita.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Ezekiel Ngeleja alisesema Silaha hiyo aliikuta Nyuma ya nyumba yake usiku wakati akienda kujisaidia ikiwa imetelekezwa na mtu anayesadikiwa kuwa jambazi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni