NA VICTOR BARIETY,GEITA 28/06/2015
BAADHI ya wakazi wa
jimbo la Geita Wilayani Geita,wamekana kufiwa na mbunge wao na kwamba marehemu
Donald Kelvin Max hakuwa mwakilishi wao bali wa Dar Es Salaam Kinondoni
alikozikwa huku chama cha mapinduzi mkoa wa Geita kikidai hakuna kanuni
zinazolazimisha mbunge kuzikwa kwenye jimbo lake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Gazeti hili,ikiwa ni
siku moja tangu mbunge wao kuzikwa,baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa pamoja
na wananchi huku wakionekana kukerwa na
jambo hilo walidai kuwa,wanachojua mbunge wao yuko hai na iwapo angekuwa
amefariki dunia angeletwa Geita kuagwa na wananchi wake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita Kamanda
Alphonce Mawazo akitoa maoni yake alisema‘’Maoni yangu ni kwamba tumehadaiwa,mimi
nilitoka mbeya kumzika mbunge wangu nikiwa sina shaka atazikwa Geita,kumbe
tulichagua tulichagua mtalii na ndiyo maana alitelekeza jimbo kwa muda mrefu
akiwa hajaanza kuugua maradhi yanayomsumbua’’
‘’Mbunge ni lazima awe na uhusiano wa ardhi ya pale
anapowakilisha,awe na wajomba,dada,shangazi,babu zake, watu aliocheza nao utotoni,aliosoma
nao,angalu awe anaguswa na damu ya pale,lakini
sisi wana Geita tulichagua kwa ushabiki na hatukujua kwamba tulichagua
mtalii’’
‘’Msiba huu umetufumbua macho na umetufundisha mambo mengi kwamba inatubidi tutambue kwamba Ubunge ni
Uchifu na Chifu hawezi kutoka eneo jingine,lazima atoke eneo lilelile
alilozaliwa maana kama mimi nilitegemea niwape pole ndugu zake,mama,mke wake na
ndiyo maana nikatoka Mbeya kuwahi mazishi harafu nikakuta hata harufu ya msiba
hakuna’’
‘’Kwa kweli wana Geita tumejisikia vibaya na sisi wananchi
tujifunzekwani na maendeleo hayaji kwa
kuchagua mtu asiye mkazi,kwani angekuwa mkazi ningempa mkono wa pole shangazi yake lakini hakuwepo,nimekuja Dar
napo sikufanikiwa maana sikujua hata msiba uko wapi’’alisema Mawazo.
‘’Mwaka 2010 niliamka
alfajiri ajili ya kuwahi foleni ili nimchague mbunge wangu
Max,nikafanikiwa..nilivyosikia kwamba amekufa sikuamini ikanibidi nianze
kutafuta msiba ulipo hadi mtaa wa katoma wanakodai ni nyumbani kwake’’
‘’Lakini hakukuwa na dalili za msiba zaidi ya mikusanyiko ya
wanaojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa
BVR,lakini wakati nikiendelea kuhangaika nijue msiba ulipo ndiyo nilipoelezwa
msiba uko Dar na atazikwa huko..hii imetudhalilisha sana wakazi wa Geita’’alisema
Fidelis Kanani mkazi wa Nyerere Road.
Zephania Mussa ambaye ni mkazi wa mtaa wa Nyanza kalangalala
mjini Geita,alisema ‘’Sisi Geita walishatudharau maana watu wa kuja ndiyo
wanachukuwa uongozi,mfano marehemu Max alitudanganya ni mkazi wa
Geita,tutamchagua tena nkwa kishindo tukiamini ni mwenzetu’’
‘’Kitendo cha mbunge wetu kuzikwa nje ya hapa na bila kuagwa
na waliomchagua kimetuuma sana na huu ndiyo mwisho kwa wanaGeita kuendelea kuwa
shamba la bibi,kwa sasa mtu atakayekuja kutuomba ridhaa ya kutuongoza tutamtaka
atupeleke nyumbani kwao,tujuwe ukoo wake na mpaka alipozikwa babu yake maana
tulkijipanga tumzike mbunge wetu kwa heshima zote kumbe anazikwa Dar imeumiza
sana nasoi tunasema waliomzika ndiyo waliomchagua wetu hajafa bado’’alisema
Mussa.
‘’Sisi kam wanageita
hili jambo limetuchanganya na ndiyo maana tunasema hatujafiwa na mbunge wafiwa
ni wakazi wa Dar,haiwezekani mtu tuliyemwamini kama mwakilishi wetu azikwe
kimyakimya sisi tuliopigwa mabomu ajili yake tusimuage na kwa nini azikwe
huko,inamaana alitudanganya ni mkazi wa Geita ili hali sivyo?’’alihoji Lucas
Charles mkazi wa mtaa wa Moringe.
Neema Steven Chozaile mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Geita alidai
kuwa,kitendo kilichofanywa na chama cha mapinduzi cha kuruhusu mbunge wa Geita
kuzikwa kimyakimya jijini Dar kimewafumbua macho wananchi na kwamba safari hii
hawatafanya makosa katika kuchagua mwakilishi wao.
‘’Tumepata fundisho kwamba tunapochagua mtu tuwe
makini,tunayemtambua alipozaliwa,ni mtoto wa Fulani maana haiwezekani mbunge wa
Geita asiletwe hapa akaagwa na waliomchagua tena kwa kura nyingi,kama CCM
wanaruka na helkopita kuhudhuria sherehe za mtia nia Monduli walishindwa
kutumia usafiri huo kuleta maiti ya mbunge wetu akaagwa hapa kisha wakamzika
watakapo,ndiyo maana tunasema huyo hakuwa mbunge wetu bali wa Dar alikozikwa’’alisema.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita,Joseph Kasheku Musukuma
alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo alidai kuwa,maiti ni ya familia ya Max na
hakuna kanuni kwenye chama chao cha Mapinduzi(CCM) zinazowalazimishwa aagwe na azikwe
eneo alilokuwa akiliwakilisha kama Mbunge.
‘’Anayehoji kwa nini Mbunge wao hakuzikwa Geita,mwambie kuwa
maiti siyo ya ccm ni ya familia ambayo ndiyo ilitoa ratiba ya wapi azikwe,mi
sidhani kama kuna sababu ya yeye kuzikwa Geita wakati kwao ni Dar es Salaam na
ndugu zake wengine wamezikwa huko,kama wanasema walimchagua kwa kishindo na
wanashangaa kuona hakuzikwa Geita waulize wakati anaumwa nani aliyekwenda
kumsalimia kwa kishindo?’’alisema Musukuma
Mbunge Max alifariki juni 23 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako
alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi(ICU)kwa zaidi ya mwaka
mmoja akisumbuliwa na kansa ya Ubongo kwa zaidi ya miaka mitatu ambapo
alipatiwa matibabu nchini India kabla ya kurudishwa hapa nchini. Alikuwa mbunge
wa jimbo la Geita tangu mwaka 2010 hadi mauti yanamkuta na amezikwa juni
27,2015 makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni