Watu 227 wameripotiwa kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu mwaka 2012/13 kwenye Maeneo ya Migodi ya wachimbaji wadogo katika wilaya za Kahama mkoani Shinyanga na Geita mkoani Geita.
Mwandishi Victor Bariety akiwa kazini
Takwimu
hizo zinatokana na Utafti ulifanywa Mwishoni mwa mwaka jana kwa
kushirikisha wadau wa Afya likiwemo shirika la Kimataifa la
Uhamiaji(Internation Organization For Migration -IOM),wachimbaji wadogo
na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Taarifa
ya Utafti huo iliwasilishwa jana(Alhamisi) kwenye mkutano mkuu wa Wadau
hao uliofanyika jijini Mwanza ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa azimio la
nchi za Kusini mwa Afrika SADC la kuthibiti ugonjwa wa kifua kikuu
kwenye maeneo ya Migodi.
Akiwasilisha taarifa
ya utafti uliofanyika kwenye migodi ya Kalole na Mwaziba wilayani Kahama
Mshauri wa Afya wa Mgodi wa ACCACIA Dk.Zumbe Musiba alisema,kuwa watu
54 wameripotiwa kuugua ugonjwa wa Kifua kikuu(TB)katika maeneo hayo.
Alisema
watu hao wameripitiwa kuugua TB baada ya kufikishwa kwenye vituo vya
Afya vya kata za Lunguya na Chela kupima Afya zao kutokana na kuishi
katika migodi ambayo mazingira yake ni machafu yenye vumbi kali na
matumizi ya zebaki bila kuwa na tahadhari.
Dk.Musiba
alisema asilimia 50 ya kesi za Ugonjwa wa Kifua kikuu zilizoripotiwa
katika maeneo hayo zina uhusiano mkubwa na Maambukizi ya Virusi vya
Ugonjwa wa Ukimwi.
"Kati ya watu
tuliowahoji,Utafti unaonyesha kuwa wengi hawajui dalili za TB hata
viongozi wao hawajui dalili na chanzo cha Ugonjwa huo,Tumeona chanzo cha
ugonjwa huo ni mwingiliano mkubwa wa watu,Vumbi linalotokana na
uzalishaji wa mawe ya dhahabu,Nyumba finyu zisizopitisha hewa"alisema
Dk.Musiba.
Aidha Mratibu wa mpango wa Taifa wa
Kuthibiti Kifua Kikuu na Ukoma Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii,Dk.Alln Tarimo amesem katika Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi
ya Gold Crest kwamba katika utafti uliofanyika Katika Migodi miwili ya
Nyakagwe na Mgusu wilayani Geita unaonyesha watu 172 wameripotiwa kuugua
TB.
Alisema katika Mgodi wa Nyakagwe watu 63
waligundulika kuwa na Ugonja wa TB Mwaka 2012 na mwaka 2013
walioripotiwa kuugua ugonjwa huo ni watu 62.
Dk.Tarimo
aliongeza kuwa katika Mgodi wa Mgusu waliogundulika kuwa na TB mwaka
2012 ni watu 17,na idadi hiyo iliongezeka hadi kwa mwaka 2013 ambapo
waliogungulika kuwa na ugonjwa huo ni watu 30.
Hata
hivyo alifafanua kuwa pamoja na Nyakagwe kuwa na kituo cha Afya hakina
huduma ya Kupima ugonjwa wa Kifua Kikuu na hivyo wanannchi hutembea
umbali wa kilomita 25 kwenda kituo cha Afya Bukoli.
"Tulipofika
Mgusu hapakuwa na kituo cha Afya wala huduma ya Vyoo hakuna hatua hiyo
huwalazimu wananchi wa maeneo hayo kusafiri umbali wa kilomita 23 hadi
25 kwenda kupata tiba hiyo kwenye Hospitali ya wilaya ya Geita na Kituo
cha Afya Nyankumbu"alisema Tarimo.
Mganga Mkuu
wa wilaya ya Geita,Dk.Noel Makuza alisema serikali kupitia idara ya Afya
wilaya haijapeleka huduma ya Kituo cha Afya katika kijiji cha Mgusu
chenye wachimbaji 9,324 kutokana na kijiji hicho kutotambuliwa.
Alisema
Mgusu ni kijiji ambacho hakijasajiliwa na kwa kuwa serikali ipo kwenye
mchakato wa kukisajili kitapata huduma stahiki zinazotolewa na serikali
ikiwemo huduma ya Afya.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni