Ijumaa, 8 Januari 2016

usafi

swala la usafi nchini liwe endelevu,kwasababu mazingira kwa hivi sasa yameonekana kuwa safi zaidi na wananchi wanajitahidi sana ,sijui kwasababu wanaogopa faini au la? haya sasa kwazi kwenu

Jumapili, 30 Agosti 2015

MWANAJESHI MBARONI KWA MAUAJI GEITA

Jeshi la polisi Mkoani Geita limemkamata mstaaf wa jeshi la wananchi Tanzania kikosi cha Komando sajent Mathias Christopher  Etta(55)kwa tuhuma za mauaji ya mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu.

Etta pia ni msimamizi msaidizi wa kampuni ya ulinzi ya (Nguvu moja security service) inayofanya shughuli zake za ulinzi kwenye mgodi wa madini wa Bacreef uliopo maeneo ya Lwamgasa mkoani hapa.

Sajent Etta alitiwa nguvuni jana majira ya saa 8 mchana kwenye kituo kidogo cha polisi cha Bacreef baada ya mwili wa  marehemu Yona Onesmo (35) ambae ni mkazi wa kijiji cha Isingiro kata ya Lwamgasa na mchimbaji mdogo kukutwa umetupwa pembezoni mwa barabara karibu na daraja la kijiji cha Mnekezi umbali wa kilomita  (2) kutoka  Lwamgasa na kilomita takribani  (15)kutoka Hospitali ya Katoro alikokua amepelekwa kupatiwa matibabu.

Imeelezwa na mashuhuda wa tukio hilo kuwa,baada ya  kupigwa usiku wa kuamkia julai 30 mwaka huu na walinzi wa kampuni ya( Nguvu moja) kwa kosa la kukutwa wanachimba kwenye eneo lililozuiliwa la mgodi wa Bacreef alikimbizwa hospitalini kabla ya mwili wake kukutwa pembezoni mwa Barabara itokayo Katoro kwenda Lwamgasa  majira ya saa nne asubuhi baada ya wakazi wa kijiji cha Mnekezi kupewa taarifa na wapita njia ukiwa bado una (Kanyura) za Hospitali zinazotumika  kutundikia drip za maji.

 “Kiukweli Katoro  kwenda kutibiwa”alisema afande Samweli Yusuph wa kituo hicho  aliyeutambua mwili huo baada ya kufika eneo la tukio.nashangaa amefikafikaje hapa kwani jana mimi nimewapeleka Hospitali ya

 Mganga mkuu wa Hospitali ya Katoro Dk Daniel Izengo alionyesha kushangazwa na taarifa  hiyo kwani alikua bado hajapokea taarifa yakupotea kwa mgonjwa hospitalini hapo,licha ya ( postmotam)yaani kikao cha wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwa tayari kilikuwa kimeshafanyika.

Hali hiyo ilimlazimu Dk,Izengo kumtafuta mhudumu aliyekuwa zamu Dk,David Mgalula ili kuzungumzia kizungumkuti hicho,akitolea ufafanuzi mhudumu huyo alikili kuwapokea wagonjwa hao wawili Bwana (Onesmo na Ndagicheye) nakusema kuwa hali ya Bw,Onesmo haikuwa nzuri kwani Marehemu alidai kuwa anajisikia maumivu makali tumboni.

“Nikweli niliwafanyia uchunguzi wa awali (Physcal chekup)nikabaini walikua na michubuko mikononi,usoni pia walikua  wamevimba joint ila marehemu alidai kuwa tumbo linamuuma nilimwandikia sindano za masaa 6 aina ya(X-pen) Sindano za Tetenasi na dawa zakumeza aina ya (Dicrofenaki)kila baada ya masaa 8 pamoja na drip,mwenzake aliruhusiwa kwani alikua anajisikia vizuri,sasa nashangaa kwanini marehem aliamua kutoroka,labda alihofia kushitakiwa na Mgodi wa Bacreef”alisema Dk huyo.

Kwa upande wa Sajent Hamis Kabonga ambaye ni msimamizi mkuu wa kampuni ya ulinzi ya (Nguvu moja security service ) alikiri kushikiliwa kwa msaidizi wake nakuongeza kuwa kukamatwa kwake kunatoka na utata wa kifo cha Yona onesmo ambae alikua nimiongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa julai 30 saa 11 kwa ajili ya  kufikishwa mahakamani mara baada yakutibiwa.

Hata hivyo hakuwa tayari kuzungumzia uwepo wa migogoro ya mara kwa mara kati ya kampuni hiyo ya uchimbaji ya Bacreef na wananchi wanaozunguka mgodi huo kwa madai kuwa msemaji wa kampuni hiyo yuko safarini hadi pale atakaporejea.

Aidha uchunguzii wa gazeti hili umebaini kuwa,licha ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita kukutana na pande hizo mbili mwanzoni mwa mwaka huu kati ya April na Mei mwaka huu ili kutatua migogoro hiyo,bado matukio yenye utata yanaendelea kujitokeza mgodini hapo.

Kwa upande wake kaimu kamanda wa polisi Mkoani Geita,Peter Kakamba amethibitisha kushikiliwa kwa mstaaf huyo wa jeshi la wananchi Tanzania  kwa mahojiano zaidi.

MWISHO.                      

PICHA ZA MAFURIKO ZAIDI MKUTANO WA LOWASSA JANGWANI

Usipitwe...Jiunge nami Hapa Niwe Nakutumia Habari Moja Kwa Moja Mara tu Zikitokea .

Mgombea urais wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi UKAWA Mh.Edward Lowasa ameongoza maelfu ya wananchi kuzinduzi rasmi kampeni za vyama hivyo katika uwanja wa jangwani huku akiwataka wataanzania kuhakikisha wanapokea mabadiliko kwa amani kwani kwa sasa hayakwepeki.

Akizungumza na maefu ya wananchi katika uzinduzi huo Mh.Lowasa ambaye amesema akichaguliwa kuwa raisi atahakikisha sekta zote ambazo zimezorota kutokana na kukosa usimamizi ikiwemo Elimu,Kilimo,na sekta ya usafirishaji ukiwemo wa reli na Anga.



Baadhi ya mawaziri waliokihama chama cha mapinduzi akiwemo Mh.Fredrik Sumaye na Laurence Masha ambao pamoja na kumpongeza Mh.Lowasa kwa kuongeza mabadiliko wamesema waliyatamani siku nyingi lakini alishindwa kwa sababu ya mfumo ulioandaliwa kwa makusudi ya kuwatia hofu na kuwatisha huku wakielezea baadhi ya maovu yanayofanyika chini ya serikali ya CCM.

Kwa upande wake mgombea mwenza Mh.Duni Haji amesema maelfu ya wananchi na viongozi wanaendelea kuunga mkono mabadiliko ni ishara ya kutosha kuonyesha kuwa wamechoshwa na uonevu na mabavu ya serikali ya CCM.

Ukafika wakati wa viongozi mbalimbali wa UKAWA wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Fereeman Mbowe ambao wamesema dalili ya kwanza ya kuonyesha kuwa viongozi wa CCM hawathamini wananchi ni kujifanya maskini huku wakificha utajiri wao.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI

































































HOTUBA YA MGOMBEA URAIS WA CHADEMA MHESHIMIWA LOWASSA


Usipitwe...Jiunge nami Hapa Niwe Nakutumia Habari Moja Kwa Moja Mara tu Zikitokea



HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015
Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu

  1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
  2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.
  3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
    1. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
    2. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.
    3. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
    4. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha.
  4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa.
  5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa.
  6. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora.
  7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa.
  8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.
  9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.
  10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka
  11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya
  12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi.
  13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi.
Ndugu watanzania

  1. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
  2. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia.
  3. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.
  4. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:-
    1. Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
    2. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
    3. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
    4. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira
    5. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
  5. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-

  1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira.
  2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
  3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
  4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
  5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi.
  6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia.
  7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata

AFYA 

  1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii
  2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.
  3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
  4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
  5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.
  6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.

ARDHI, MAJI NA KILIMO


  1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
  2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
  3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
  4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
  5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.
  6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga miundombinu husika.
  7. Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa
  8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima na wafugaji.
  9. Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
  10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
  11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.

MIUNDOMBINU

  1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
  2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
  3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
  4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
  5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
  6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya Watanzania

VIWANDA

  1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
  2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
  3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
  4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda

UCHUMI

  1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
  2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya biashara na kodi endelevu.
  3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
  4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
  5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila kujali wanapotoka.
  6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima wenyewe ikiwa na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa kushirikiana kujenga nyumba bora
  7. Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji wa viwanda vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na vyuo vya ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.
AJIRA

  1. Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri
  2. Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha ajira kwa wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na kuzipa unafuu wa kodi ili zikue kwa haraka.
  3. Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI 

  1. Serikali itashiriki kikamilifu katika uzalishaji wa nishati
  2. Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na ubia kati yao na wageni.
  3. Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa umeme wa maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe kipaumbele namba mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele namba tatu na umeme wa urana kipaumbele namba nne.
  4. Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye usambazaji wa huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga masoko ya ndani, ya nchi jirani na ya nchi za kigeni.
  5. Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya nishati na madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia maboresho.
  6. Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa zake kwenye raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini kama rehani kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya mabomba ya gesi.
  7. Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi kwa wazawa wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa wageni wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.

  1. Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya kodi isiyo lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza kwenye kuongeza thamani ya raslimali zake za madini.
  2. Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni

MALIASILI NA UTALII

  1. Tutasimamia uvunaji na matumizi ya rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi hiki na kijacho
  2. Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha utunzanji wa hifadhi za taifa na mazingira
  3. Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na kuimarisha mafunzo
  4. Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion mbili ifikapo 2020.



UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA RAIA

  1. Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za msingi za wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na viongozi, Bunge na Mahakama.
  2. Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya sheria kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti jela kwa sababu za kisiasa.
  3. Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa kusimamia utoaji wa haki.
  4. Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI

  1. Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
  2. Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika Sekta ya Umma
  3. Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
  4. Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika sekta ya Umma na binafsi
  5. Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
  6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
  7. Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI

  1. Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali kwa kupitia upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi asilia ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio stahiki.
  2. Serikali itaanzisha Wizara maalum itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
  3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na mapato yake.
  4. Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
  5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa forodha na kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni ya fedha yanayopotea kila wiki.
  6. Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu wa kulipa kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti makusanyo ya kodi tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama afya na elimu kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO 

  1. Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE

  1. Wanawake watapewa fursa na haki sawa katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
  2. Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya uzazi
  3. Tutaimarisha elimu ya watoto hasa wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto wadogo.
  4. Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia hamsini ifikapo 2020.
  5. Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya familia na jamii zao.

SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO

  1. Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na michezo
  2. Tutarudisha viwanja vya michezo vilivyovamiwa
  3. Tutafuta kodi zote za vifaa vya michezo.
  4. Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
  5. Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha
  6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
  7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA

  1. Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa wenye tija na Ujirani mwema.
  2. Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.
  3. Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa Mataifa.
  4. Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi shiriki.
Ndugu Watanzania
Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo

  1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.
  2. Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi jasho lenu na uwezo wenu wote ili kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka utawala wa CCM unaodumaza uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika kuondoa umaskini.
  3. Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za uchaguzi kwa kupewa pesa au vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM. Ukikubali basi umeuza pia haki na sauti yako ya kuwalalamikia walio madarakani. Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague mabadiliko.
  4. Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na kutenda tofauti. Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba hatuna dharura ya maendeleo. Kwanza tuanze kwa kufanya mabadiliko na tujiamini kuwa sisi kama Taifa tunaweza. Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka kwao.
  5. Tuwe taifa linalotumia raslimali zake kujiendeleza na siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana katika nchi yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na kuvaa umaskini kama joho la fahari.
  6. Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na CCM. Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa miaka thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi. Tukatae hadaa. Miaka hamsini ya CCM imetosha.
  7. Tunaamani kwamba tutashinda kwa sababu Watanzania mpo nyuma yetu. Watanzania mmeamua kuleta mabadiliko. Kura yako ndiyo itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda kura yako. Wakati wa mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana

ANGALIA HOTUBA NA MAFURIKO YA LOWASSA JANGWANI - AUGUST.29.2015 | AZAM TV

Jumanne, 11 Agosti 2015

around the corner

Njia ya Uzima -Makongoro Choir

LULU-Mtoni Evangelical Choir

AIC MAKONGORO CHOIR-MWOKOZI KAFUFUKA

MSHIPI - KWAYA KUU YA MT. CESILIA, ARUSHA

BEST OF MALINDI CATHOLIC KENYA CHOIR LATEST COLLECTION FULL ALBUMS PLAYLIST

Coca-Cola Billion Reasons to Believe: Churchill - Laughing All The Way...

Bhudagala Mwana malonja_Ng'wamba

WAGOMBEA SABA CCM GEITA KUMFUATA LOWASSA?



NA VICTOR BARIETY,GEITA

Wagombea saba wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi wamepinga matokeo ya uchaguzi kwa madai kwamba yamegubikwa rafu na karatasi za kupigia kura kutokuwa na picha za wagombea huku wakitishia kufanya maamuzi magumu iwapo malalamiko yao yatapuuzwa.

Jumatano, 22 Julai 2015

MAKAMU WA RAIS BILAL ASISITIZA AMANI YA NCHI

NA VICTOR BARIETY,GEITA

MAKAMU wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, amewataka waislam na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanadumisha amani na umoja ulioachwa na waasisi wa taifa hili hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

WAUGUZI WAMKAANGA MGANGA MKUU MBELE YA MWENYEKITI WA TAIFA,WAMKATAA

NA VICTOR BARIETY,GEITA

WAUGUZI  na wahudumu wa afya katika  hospitali ya wilaya ya geita wamemkataa mganga mkuu wa hospitali hiyo  Dkt. Noel Makuza   kwa madai kuwa amekuwa akitumia ubabe pamoja na lugha chafu kwa wafanyakazi hao.

Wakitoa malalamiko hayo jana  mbele ya Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa afya (TUGHE) Taifa Archie Mntambo, watumishi hao wa afya walisema kuwa Dkt. Makuza amekuwa kikwazo kwao, mbali na kutoa lugha chafu  pia ameshindwa kuidhinisha fedha za malipo  yao mbalimbali, yakiwemo malimbikizo ya fedha za likizo na malipo kwa saa za ziada kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa TUGHE tawi la hospitali ya wilaya, Mary Muntu  alisema kuwa kiongozi huyo wa hospitali hana sifa za kuongoza watumishi wanaohudumia wagonjwa katika hospitali hiyo kutokana na kukosa hekima na busara za kiuongozi katika kuongoza watu walio chini yake.

Muntu alisema kuwa kutokana na tabia yake ya  ubabe na lugha chafu kwa watumishi wenzake hali hiyo inasababisha kudhorota kwa huduma ya afya siku hadi siku.

“Hakuna maelewano mazuri baina ya mganga mkuu na wafanyakazi wengine..uongozi wa hospitali HMT unapopeleka malalamiko kwa uongozi uliopo chini yake CHCMT hakuna majibu ya kulidhisha ambayo yanatolewa kutokana na kutumia nafasi yake hiyo kwa ubabe”alisema Muntu.

“Nilibambikizwa nikakamatwa na rushwa ya sh. 1000 iliyotengenezwa na Dkt. Makuza kwa sababu nafuatilia maslahi ya watumishi wenzangu..lakini kwa kuwa siku zote haki ya mtu haipotei nilishinda hiyo kesi mahakamani baada ya kukaa zaidi ya mwaka mmoja nikiwa nje ya kazi nimesimamishwa…mbali na hilo pia anatabia ya ubabe na lugha chafu kwa watumishi,amefuja fedha za watumishi za likizo, malipo ya saa za ziada kazini’’aliongeza Muntu.

Thabitha Shiduki Muuguzi wa hospitali hiyo alisema tangu aajiliwe hospitalini hapo, hajawahi kulipwa fedha zake za likizo licha ya fomu zake kuzipeleka kwa DMO lakini zimekuwa zikitupiliwa mbali pasipo kushughulikiwa.

“Kuna tatizo kubwa hapa sijawahi kulipwa fedha yangu ya likizo, pamoja na hayo mimi binafsi sina mahusiano mazuri na mganga mkuu kutokana na lugha zake chafu hana ushirikiano hata kidogo ofisi yake naiona kama kituo cha polisi,alisema Shiduki.

Kutokana na hilo, wauguzi pamoja na wahudumu wa afya, kwa pamoja walimuomba Mwenyekiti huyo wa tughe taifa Archie Mntambo awasaidie kumuondoa DMO huyo kwasababu amekuwa ni kero hospitalini hapo.

Naye Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Adamu Sijaona alikiri kuwepo kwa changamoto hizo hospitalini hapo na kwamba malalamiko ya watumishi wenzake amekuwa akiyafikisha panapohusika.

‘’Stahiki za watumishi zipo kisheria, kuna likizo, mavazi ya wauguzi, matibabu, malipo ya ziada kuna kupandishwa vyeo na nyumba za madaktari..kakweli kuna tatizo kwa namna moja ama nyingine,’’alisema Dkt. Sijaona.

Kufuatia hali hiyo Mwenyekiti huyo wa TUGHE taifa Archie Mntambo alimwagiza afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Geita kumpatia uhamisho mganga huyo ili kuondoa msuguano uliopo.

“Nawaomba halmashauri mlitafakari hili na ikiwezekana mpatieni uhamisho DMO..ili sasa muondoe kero zilizopo hapa kwasababu akiendelea kuwepo ufanisi wa kazi utapungua na matatizo makubwa yanaweza kutokea…waathirika wakubwa wa mgogoro huu ni wananchi na si watumishi,’’alisema Mntambo.

Hata hivyo Mganga Mkuu Dkt. Noel Makuza hakuweza kutokea katika kikao hicho cha watumishi wa afya wa hospitali hiyo kwasababu  ambazo hazikuweza kujulikana mara moja na alipopigiwa simu yake ya kiganjani hakupokea na wala hakujibu ujumbe wa maandishi aliotumiwa

Mwisho.